MHE.MWINJUMA ATOA AGIZO KWA TPBRC
service image
11 Jan, 2025

Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma ametoa maagizo kwa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBRC) kuweka vigezo vya mabondia kuingia kwenye ngumi za kulipwa.

Maagizo hayo ameyatoa leo tarehe 11 Januari 2025 jijini Dar es salaam alipokutana na mapromota wa ngumi za kulipwa kwa ajili ya kujadili mambo mbalimbali yanahusiana na mchezo huo.

“TPBRC mnatakiwa kuweka vigezo vya  muda wa bondia kucheza ngumi za kulipwa, awe amecheza ngumi za ridhaa,  kwa muda gani au mapambano mangapi anatakiwa kucheza kuweza kuingia katika kigezo hicho"

"Hivi sasa mabondia wengi wanaingia moja kwa moja kulipwa bila kupitia ngumi za ridhaa,  TPBRC nahitaji kupata majibu Januari 15, 2025,  mapambano mangapi wanatakiwa kupitia,” amesema Mhe.Hamis Mwinjuma

Katika hatua nyingine amewataka Bazara la Michezo la Taifa (BMT), kufuta utaratibu wa kutoa kibali cha kusafiri kwa bondia pale anapokuwa uwanja wa ndege.

“Vibali vyote vya kusafiri vifuate utaratibu,  mtu akienda uwanja wa Ndege halafu anapiga simu au bado siku chache kwenda safari kwa ajili ya kwenda katika pambano hakuna kutoa, huruma hiyo ife,” amesema Mhe. Mwinjuma.