BINGWA WA BAISKELI KUTOKA POLAND KUWEKA REKODI TANZANIA
service image
01 Apr, 2023

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Balozi Dokta Pindi Chana amempongeza Bingwa wa mashindano ya Baiskeli Duniani kutoka nchini Poland Mike Leszek ambaye anataka kuweka rekodi ya Dunia ya Guiness kwa kupanda na kushuka Mlima Kilimanjaro kwa saa 24.

Mhe.Chana ametoa pongezi hizo leo tarehe 1 Aprili, 2023 alipokutana na Bingwa huyo , ambaye amekuja nchini kwa ajili ya maandalizi ya tukio kubwa la kupanda Mlima Kilimanjaro mwezi Septemba au Oktoba mwaka huu.

Aidha Mhe. Chana amesema ujio wa Bingwa huyo imedhihirisha kuwa Tanzania ni nchi ya Amani, Upendo na ina ushirikiano nzuri na nchi zingine, hivyo wanamichezo mbalimbali Duniani wanavutiwa kuja nchini, jambo ambalo lina tija kubwa kwa Taifa.