MSITHA ASKED TWALIPO TO CONTINUE COOPERATION
service image
19 Mar, 2025

Katibu Mtendaji wa BMT Bi. Neema Msitha leo Machi 19, 2025 ameiomba Shule ya mafunzo ya michezo na utimamu wa mwili kupitia kwa Mkuu wake Kanali John Thomas Nyanchoha pamoja na wakufunzi wa Michezo kutoka kambi ya Twalipo Mgulani kuendelea na ushirikiano na Baraza pamoja na vyama vya michezo.

Msitha amesema hayo, wakati walipomtembelea Ofisini kwake kwa lengo la kumuaga kama mdau wao Mkuu wa Michezo nchini wanayeshirikiana naye, wakieleza kuhamisha shule hiyo kuelekea 'Sokoine Barracks' Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha.

"Sisi tunawategemeeni sana nyinyi katika mafanikio ya michezo, nitaendelea kusema kwanini tunadhani huko kwenu tunaweza kufanikiwa zaidi, kwanza suala la utimamu wa mwili, miundombinu na uwezeshwaji,"alisema Msitha.