BMT KUWANOA WALIMU WA MICHEZO KUTOKA SHULE TEULE 56 ZA MICHEZO NCHINI

02 Nov, 2022
Baraza la Michezo la Taifa (BMT) linataraji kuendesha mafunzo kwa walimu wa michezo kutoka katika shule teule 56 za michezo nchini kwa lengo la kuongeza ujuzi kwa walimu hao ili kutoa fursa kwao kuendelea kuibua na kuendeleza vipaji zaidi shuleni.
Mafunzo hayo yanataraji kuanza tarehe 3 hadi 9 Novemba katika moja ya kumbi za uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.