BMT YAKABIDHI TIKETI ZA ZAIDI YA MILIONI 50 KWA SPECIAL OLIMPIKI
service image
22 May, 2023

Serikali kupitia Baraza la Michezo la Taifa (BMT) limekabidhi tiketi za ndege kumi na tano (15) zenye thamani ya Milioni hamsini, mia tatu tisini na sita mia saba sabini na tano (50, 396, 776) kwa timu ya Special Olimpiki.

BMT imetoa tiketi hizo leo Mei 22, 2023 kuiwezesha timu hiyo kwenda kushiriki mashindano ya dunia yanayoratajiwa kufanyika kuanzia tarehe 26 hadi 29 June, 2023 Berlin nchini Ujerumani.

Timu hiyo ambayo ipo kambini Mkoani Arusha chini ya ufadhili wa kituo cha Sibusiso Foundation linaloshughulika na kundi hilo, watagwa na Baraza Juni 11 kabla ya kusafiri tarehe 12 June, 2023 kuelekea nchini Ujerumani.

Msafara katika safari hiyo utahusisha watu 27 kutoka pande zote za muungano ambapo tiketi na gharama zingine ni kwa ufadhili wa wadau wengine wakiwemo Azam media, Sibusiso na ASAS Group.