BMT YATOA TUZO KWA RAIS SAMIA
service image
17 Mar, 2023

Baraza la Michezo la Taifa (BMT) limetoa tuzo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kuonesha na kutambua mchango mkubwa aliotoa katika maendeleo ya michezo nchini.

Tuzo hiyo imekabidhiwa Machi 17, 2023 kwa Waziri mwenye dhamana ya Michezo Dkt. Pindi Chana katika usiku wa tuzo kwa wanamichezo, tukio lilifanyika jijni Dar es salaam.