BMT YAWATAKA TGU,TLGU NA KLABU YA GYMKHANA KUIMARISHA USHIRIKIANO

10 Feb, 2023
Baraza la Michezo la Taifa (BMT) ikiwakilishwa na Afisa Michezo Benson Chacha leo tarehe 10 Februari, 2023 imewakutanisha viongozi wa vyama vya mchezo wa Gofu (TGU) na chama cha mchezo huo cha Wanamake (TLGU) pamoja na Klabu ya Gymkhana na kufanya nao mazungumzo kwa nia ya kuimarisha ushirikiano kwa maendeleo ya mchezo huo nchini.