BONDIA KASSIM MBUNDWIKE AMEFUZU HATUA YA NUSU FAINALI KATIKA MASHINDANO YA JUMUIYA YA MADOLA

04 Aug, 2022
Bondia mwingine wa Tanzania, Kassim Mbundwike, amtwanga kwa “Knockout” bondia wa Samoa Ah Tong na kutinga hatua ya nusu fainali.
Tanzania sasa ina uhakika wa Medali Tatu ile ya Fedha ya Alphonce Felix Simbu katika mchezo wa riadha na mbili za mabondia wa ngumi za Ridhaa waliofika hatua ya nusu fainali.
Kwa mujibu wa taratibu na kanuni za mashindano hayo mabondia wanaofika fainali wote wanapata medali na zitatofautiana kutokana na matokeo ya nusu na fainali yenyewe.