WITO KWA VIONGOZI WA MCHEZO WA KABADDI

01 Sep, 2023
Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bi. Neema Msitha amewataka Viongozi wa Chama cha mchezo wa Kabaddi nchini kuhakikisha wanawatumia vyema makocha kutoka India kwa kuwapeleka Mikoa mingi zaidi ikiwemo ya Zanzibar.
Rai hiyo ameitoa leo Septemba Mosi, 2023 baada ya kupokea ugeni wa Makocha wawili wa mchezo huo walifika nchini kupitia chama cha mchezo huo ili kuja kufundisha makocha na timu ya taifa ya mchezo huo.