CHANGALAWE ATINGA FAINALI KIBABE KUFUZU OLIMPIKI YA PARIS 2024

15 Sep, 2023
Nahodha wa Timu ya Taifa ya Ngumi NGORONGORO BLACK RHINOS (Faru weusi wa Ngorongoro) Yusuf Lucas Changalawe amefanikiwa kuingia hatua ya fainali ya mashindano ya kufuzu Olimpiki ya Paris 2024 kwa Bara la Afrika dhidi ya Younes Nemouchi kutoka Algeria.
Changalawe ameshinda kwa "Knockout" katika 'round' ya 3 baada ya kuongoza kwa pointi katika 'round' zote za pambano namba 208 katika uzani wa 80kg.