CHANGALAWE ASHINDA DHIDI YA MWENYEJI SENEGAL NA KUTINGA NUSU FAINALI
service image
13 Sep, 2023

Nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania "Faru weusi wa Ngorongoro" Yusuf Changalawe katinga hatua ya nusu fainali baada ya kushinda kwa points 4-1 dhidi ya Seydina Konate mwenyeji kutoka Senegal.

Ni katika bout no. 170 ya uzani wa 80kg ambapo sasa Changalawe ametinga hatua ya nusu fainali ambayo atacheza kesho.

Mabondia wengine wa Tanzania waliocheza awali ya leo katika hatua ya robo fainali walipoteza ambapo Abdallah Katoto dhidi ya Said Mortaji kutoka Morocco kwa points 4-1 katika bout no 166 uzani wa 51kg na Grace Mwakamele kwa RSC round ya kwanza dhidi ya Imane Khelif kutoka Algeria katika bout no. 165 uzani wa 66kg.