CHESS KUIWAKILISHA TANZANIA DUNIANI

26 Jul, 2022
Na. Najaha Bakari
Wachezaji kumi (10) wa mchezo wa Chess nchini wameondoka jana tarehe 25, ambao wamewasili leo tarehe 26 Julai, 2022 kuiwakilisha nchi katika mashindano ya 44 ya dunia yatakayoanza kesho tarehe 27Julai na kuhitimishwa Agosti 10, 2022 Chennai nchini India.
Tanzania katika mashindano hayo itawakilishwa na
wachezaji 10, wanawake 5, wanaume 5, Manahodha wawili (2) na kiongozi wa mmoja wa msafara ambaye pia atashiriki kwenye Mkutano Mkuu wa uchaguzi wa Rais mpya wa shirikisho la mchezo huo duniani (FIDE) kwa mwaka 2022-2026.