Dkt. ABBAS ASHUHUDIA MASHINDANO YA CLUB BINGWA YA NETIBOLI LIGI DARAJA LA KWANZA JIJINI DSM

12 Jul, 2022
Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi leo Julai 12, 2022 ameshuhudia Mashindano ya Club Bingwa ya Netiboli ligi daraja la kwanza yanayofanyika katika uwanja wa ndani wa Uhuru jijini Dar es salaam.
Dkt. Abbasi ameshuhudia mchuano mkali kati ya TAMISEMI na timu ya Eagle ya Ubungo ambapo TAMISEMI wameibuka washindi kwa magoli 90 -09 dhidi Eagle.
Dkt. Abbasi katika ziara yake ya kushuhudia mtanange wa Club bingwa ya mchezo wa netiboli inayoendelea katika uwanja wa ndani wa uhuru aliambatana na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Yusuph Singo