DKT. ABBASI AITAKA BMT KUWA PROGRAMU ENDELEVU

Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ameitaka menejimenti ya Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kuandaa programu endelevu za mafunzo kwa viongozi wa vyama vya michezo nchini kwa kushirikiana Chuo cha Maendeleo Malya ili kuwajenga uwezo wa kuongoza.
Rai hiyo ameitoa leo Novemba 16, 2022 wakati wa kikao na Menejimenti hiyo kupata taarifa ya utekelezaji wa maagizo tofauti ya viongozi wa juu nchini.
"Mafunzo yawe na wataalamu wabobezi lakini pia jitahidini kutafuta wataalam kutoka nchi zilizoendelea kimichezo ili waje kuwapa uzoefu viongozi wetu kuongoza taasisi za michezo"alisema Katibu Mkuu.
Vilevile ameitaka Menejimenti hiyo kwa kushirikiana na viongozi wa vyama vya michezo kuandaa mpango mkakati wa mafunzo kwa makocha na wataalam tofauti wa michezo ili nchi iwe na wataalam wa kutosha wenye kuwa na lengo la matokeo ya mbali.
"Tunahitaji wataalam ambao wapo katika ngazi ya ushindani na matokeo ya mbali siyo ya leo,"alisisitiza Dkt. Abbasi.