DKT. ABBASI NAWAPA SIKU 14 KUWASILISHA NYARAKA ZITAZOSAIDIA KUANZISHWA KWA SHERIA
service image
03 Nov, 2022

Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni Sanaa na michezo Dkt. Hassan Abbasi ametoa siku 14 kwa Idara ya Michezo, Baraza la Michezo la Taifa (BMT na Kamati ya kupambana na mbinu haramu michezoni nchini kuwasilisha nyaraka itakayowasilishwa Bungeni ili kuundwa kwa Sheria ya kupambana na mbinu na dawa haramu za kuongeza nguvu michezoni.

Dkt. Abbasi ameyasema hayo leo Novemba 03, 2022 katika hotuba yake wakati wa kufunga semina ya siku nne ilikuwa imegawanyika katika makundi matatu yenye washiriki 100 kutoka vyama vya michezo, wadau, wachezaji, maafasa kutoka BMT, Wizarani pamoja na maafisa michezo wa wilaya za Mkoa wa Dar es salaam.

Aidha, Dkt. Abbas, alisema kuwa katika kipindi hiki ambacho Rais Samia Suluhu Hassan, amekuwa akiwekeza mabilioni  kwenye michezo sio ya kukosea.   

“Kingine muhimu kwenye  mashindano  wanayoandaa vyama na mashirikisho wanapaswa  kuandaa na kuweka vifaa vinavyohitajika pamoja na kutenga bajeti kwa ajili ya kupambana na mbinu haramu michezoni,” Alisema Dkt. Abbas.

Katika hatua nyingine Dokta Abbas ameipa siku tatu kamati ya kupambana na mbinu haramu michezoni kuhakikisha wanawasilisha nyaraka za madeni ya Regional Antidoping Organization ( RADO)  na World Antidoping Agency ( WADA) ambazo ni madeni ya nyuma Wizarani.