DKT. NDUMBARO AWEKA WAZI MALENGO YA WIZARA KATIKA KULETA MABADILIKO SEKTA YA MICHEZO

Serikali kupitia kwa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Damas Ndumbaro imesema itatengeneza mfumo wa kuwa na mahakama ya usuluhisho wa migogoro katika vyama vya michezo.
Akizungumza katika mkutano wa viongozi wa vyama na mashirikisho ya michezo nchini leo Machi 06, 2024 Waziri Ndumbaro amesema mfumo huo utasaidia kutafuta migogoro na kupata mafanikio katika sekta ya michezo nchini.
Ameongeza kuwa, Wizara, Baraza la Taifa la Michezo (BMT) wataangalia kona ya ajira na uchumi, hivyo kuendelea kurasimisha michezo ya Kulipwa nchini.
"Haya ni maeneo ya kuyafanyia kazi ili kuhakikisha mafanikio ya maendeleo ya michezo yanapatikana," alisema
Dkt. Ndumbaro amesema kuwa, watakuwa na katiba ya mfano kwa vyama vyote ambapo, mchakato umeanza kwa kuunda Kamati ya kuishauri Serikali kupitia BMT ambayo itahusisha maoni ya wadau.
Alieleza kuwa Serikali itatunga kanuni za uwazi katika masuala ya vyama vya michezo ambayo itasaidia vyama kutoa taarifa za fedha za ndani na nje.
Aidha amevitaka vyama vya michezo kuwa na mpango mkakati wa maendeleo ikiwemo kuwa na ofisi na Wizara itatoa muda kwa vi HBsio na ofisi vitafutwa.