GOLI LA MAMA

13 Jun, 2024
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akiwaonesha wachezaji wa Timu ya Taifa ya Mpira wa miguu (Taifa Stars) shilingi Milioni kumi (10) za goli la Mama ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kabla ya kumkabidhi Nahodha wa Himid Mao baada ya kushinda goli 1- 0 dhidi ya timu ya taifa Zambia (Chipolopolo) mchezo wa kufuzu kombe la dunia uliochezwa Juni 11, 2024 katika uwanja wa wa Levy Mwanawasa Ndola Nchini humo.