UKAGUZI WA VIWANJA VITAKAVYOTUMIKA CHAN
service image
04 Jan, 2025

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Paramagamba Kabudi amesema Tanzania iko tayari kwa ajili ya mashindano ya CHAN na kwa sasa hatua ya kazi iliyofikia katika viwanja vyote vitatu vya mazoezi imefikia asilimia 99% ambapo nchi iko tayari kuwa mwenyeji wa mashindano ya CHAN yatakayofanyika hivi karibuni.

Waziri Kabudi ameyasema hayo Januari 04, 2025 mara baada ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ukarabati wa viwanja vya mazoezi ambavyo vitatumika kwa ajili ya mashindano ya CHAN 2025 na AFCON 2027 Dar es salaam.