MAELEKEZO YA PROFESA KABUDI KWA BMT
service image
04 Jan, 2025

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Profesa Paramagamba Kabudi amewataka Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kufanya kazi saa 24 katika kipindi cha maandalizi ya CHAN pamoja na TFF kuhakikisha maandalizi timu ili kuhakikisha ushindi unapatikana.

Profesa Kabudi ameyaseama hayo Januari 04, 2025 katika uwanja wa Meja jenerali Isamuhyo uliopo Mbweni jijini Dar Es salaam alipofanya kikao na viongozi mbalimbali walengwa kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya CHAN 2025.