WAKUFUNZI WA MCHEZO WA KABADDI

30 Aug, 2023
Wakufunzi wa mchezo wa Kabaddi waliowasili Tanzania tarehe 26 Agosti, 2023 kutoka nchini India, leo tarehe 30 Agosti, 2023 katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, wameanza programu maalum kuwafundisha wachezaji kutoka katika vilabu mbalimbali vya kabaddi nchini, kuhusu mbinu muhimu zinazotumika katika mchezo huo.