KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YAKAGUA MIUNDOMBINU YA MICHEZO JIJINI DAR ES SALAAM

15 Apr, 2023
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo imetembelea miundombinu ya michezo ukiwemo Uwanja wa Benjamin kuona ukarabati unaoendelea katika Uwanja huo pamoja na mradi wa ujenzi wa Viwanja katika eneo la Kigamboni unaotekelezwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Kamati imeridhishwa na maboresho yanayofanywa katika Uwanja wa Benjamin pamoja uwekezaji unaofanywa na TFF jijini Dar es salaam kwa maendelea ya mpira wa miguu nchini.
Kamati hiyo imetembelea maeneo hayo leo Aprili 15, 2023 ambapo waliongozwa na Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Hamis Mwinjuma, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Nicholas Mkapa na Watendaji wengine wa Wizara pamoja na Baraza la Michezo la Taifa (BMT).