KAMATI YAENDELEA NA MIKAKATI KUFANIKISHA TANZANITE

KAMATI YAENDELEA NA MIKAKATI KUFANIKISHA TANZANITE
Na. Najaha Bakari - DSM
Kamati ya maandalizi ya Tamasha la michezo kwa wanawake lijulikanalo kwa jina "Tanzanite" leo Julai 08, 2022 limeendelea na kikao cha pili cha maandalizi ya tamasha hilo la mwaka 2022 linalotarajiwa kufanyika mwezi Septemba Jijini Dar es salaam.
Maandalizi ya tamasha hilo kwa mwaka huu limelenga kuongeza idadi ya michezo pamoja na kushirikisha baadhi michezo kuchezwa kimataifa iwapo maandalizi yatafanikiwa kama inavyopendekezwa ili kuongeza hamasha na nguvu kwa wanawake kushiriki katika michezo.
Aidha, michezo inayotarajiwa kuwepo katika tamasha hilo ni pamoja na mpira wa miguu, netiboli, riadha, Wavu, kikapu kwa wenye ulemavu na kawaida, michezo ya jadi, mpira wa mikono, kabaddi, shotokan karate na mchezo wa power arts.