MAAFISA HABARI KUONGEZA HAMASA MCHEZO WA TAIFA STARS NA UGANDA THE CRANES
service image
27 Mar, 2023


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametangaza Ofa ya tiketi na usafiri kwa Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini wote wanaoshiriki kikao kazi Cha 18 kwenda Uwanjani kuishangilia Taifa Stars itakapocheza na Uganda The Cranes Machi 28, 2023 Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam, ikiwa ni mchezo wa kufuzu AFCON mwaka 2024.

Mhe. Majaliwa ametangaza ofa hiyo iliyotolewa na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa Maafisa hao, leo Machi 27, 2023 jijini Dar es Salaam, wakati akifungua kikao kazi cha 18 cha Maafisa hao kinachofanyika Ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam, ambapo Katibu Mkuu wa Wizara Ndg. Saidi Yakubu ameshiriki.

Taifa Stars itacheza na Uganda The Cranes Machi 28, 2023 ikiwa ni mechi ya marudiano baada ya kuifunga Goli 1 Kwa 0 katika mchezo wa awali uliochezwa Machi 24, 2023 mjini Ismailia nchini Misri.