MAANDALIZI YA TIMU ZA TAIFA ZA KABBADI

14 Jul, 2022
Na. Najaha Bakari - DSM
Timu ya taifa ya mchezo kabaddi leo Julai 14, 2022 imeendelea na mazoezi kujiweka sawa kuelekea katika mashindano ya Afrika yanayotarajiwa kufanyika nchini Misri kuanzia tarehe 22 hadi 29 Julai, 2022.
Wachezaji hao wa kabaddi ambao wako kambini tangu tarehe 10 Julai, 2022 katika hostel za Police college Kurasini, wameendelea kujinoa na mazoezi ndani ya viwanja vya jeshi hilo na katika uwanja wa uhuru ili kuiwakilisha nchi katika mashindano hayo.
Tanzania katika mashindano hayo itawakilisha na wachezaji 24 wakiwemo wachezaji 12 wa timu ya wanaume na 12 wa timu ya wanawake.