MAANDALIZI YA UKARABATI WA UWANJA

20 Mar, 2023
Waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Balozi Dkt. Pindi Chana na Naibu wake Mhe. Hamis Mwinjuma leo Machi 20,2023 wamefanaya ziara ya kikazi katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam,Kuona maandalizi ya Ukarabati wa uwanja huo.
Katika ziara hiyo waliambatana pia na katibu Mkuu wa wizara hiyo,Said Yakubu,pamoja na Mkandarasi Mwelekezi kutoka wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Viongozi wa Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Viongozi wa wa Sekta ya Michezo na Wataalam wa uwanja huo.