MAFUNZO YA USAJILI KWA MFUMO WA KIDIGITALI
service image
18 May, 2023

Baraza la Michezo la Taifa (BMT) linaendelea kuupinga mwingi kusambaza elimu ya mfumo wa usajili wa vyama vya michezo kidigitali ili kurahisisha huduma hiyo, ambapo, mteja atajisajili popote alipo bila kusafiri.

Tarehe 18 hadi 19 Mei, 2023 mafunzo hayo yanatolewa kwa Maafisa michezo wa Mkoa wa Morogoro sambamba na viongozi wa vyama vya michezo vilivyomo katika Mkoa huo ili wawe mabalozi wa kusambaza mafunzo hayo kwa wadau wengine ambao hawajabahatika kuyapata katika maeneo yao.

Mafunzo hayo ni endelevu ambapo Morogoro ni Mkoa wa nane (8) kufaidika, ambayo yalianzia Mkoa wa Dar es salaam, Lindi, Mtwara, Pwani, Njombe, Ruvuma na Iringa na yatafunguliwa rasmi tarehe 1
01 Julai, 2023.