MAJALA AWEKA WAZI TARATIBU ZA USAJILI

Na Najaha Bakari - Pwani
Msajili wa Vyama vya Michezo wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Riziki Juma Majala ametoa ufafanuzi wa taratibu na vitu muhimu vya kuambatisha ili uweze kusajili Shirikisho/Chama/Klabu au taasisi yoyote ya michezo nchini.
Ufafanuzi huo ameutoa leo tarehe 25 Juni, 2022 wakati wa kikao kazi cha Maafisa Michezo wa Mkoa wa Dar es salaam na Pwani kilichofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Njuweni Kibaha Mkoani Pwani.
Viambatisho muhimu ili kusajili taasisi ya michezo ni pamoja Katiba tatu, orodha ya majina ya waliokubaliana kuanzisha na muhtasari wa kikao cha makubaliano.
Aidha, katika kikao hicho Maafisa Michezo hao wamepata muda wa kuuliza maswali tofauti yaliyokuwa kikwazo katika utendaji kazi wao katika maeneo yao na kupata ufafanuzi wa kina kutoka kwa wawasilishaji wa mada tofauti kutoka BMT.
Kikao kazi hicho kimehusisha maafisa michezo wapatao kumi na tatu (13) BurwanTilusubya kutoka Halmashauri ya Kibaha, Lulu Ndali Halmashauri ya Kisarawe, Lydia A.Masenha Chalinze, Adolfina Mohamed Manispaa ya Kigamboni, Wikansia Mwanga kutoka Manispaa ya Ubungo.
Wengine ni Ramadhani Mchangule Halmashauri ya Mkuranga, Respis Bileha Halmashauri ya Kinondoni, Hassan Katuli Kibaha DC, Emmanuel Nyanda Rufiji Ingridy Kimario Manispaa ya Temeke na Adorph Halii Afisa Michezo Mkoa wa Dar es salaam na Afisa Michezo mwenyeji wa Mkoa wa Pwani Grace Buretha.