MASHINDANO YA RIADHA KWA WANAWAKE YAPAMBA MOTO KWA MKAPA.

Mashindano ya Riadha ya Wanawake (Ladies First 2023) yameanza rasmi hii leo katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es salaam huku ikishuhudiwa Medali kadhaa zikigaiwa Kwa washindi mbalimbali walioshiriki katika Mbio za kadhaa zilizofanyika hii leo.
Jackiline Sakilu, Magdalena Shauri, Jane Maige wamefanikiwa kung'ara katika fainali ya mbio za mita mbalimbali katika Mashindano hayo yaliyoanza leo kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Katika mita 10,000 Jackline kutoka Arusha amefanikiwa kuibuka mshindi wa kwanza baada ya kutumia dakika 35:51:98, huku Neema Nyaisawa wa Mara ametumia dakika 36:21:72 na Marcelina Mbua wa Arusha amemalizia nafasi ya tatu kwa kutumia dakika 36:45: 42.
Katika mbio za mita 1500 Magdalena Shauri wa Arusha ameshika nafasi ya kwanza akiwa ametumia dakika 4:25:76, huku Salma Charles wa Pwani aliyeshika nafasi ya pili akitumia dakika 4: 36:24 na nafasi ya tatu ikienda kwa Valelia Charles Wa Arusha ambaye ametumia dakika 4:40:27.
Matokeo mengine katika mita 400 Jane Maige wa Kaskazini Unguja ameshika nafasi ya kwanza kwa kumaliza kwa sekunde 55:37, huku Teresa Benard wa Kusini Unguja ametumia 57:29 na Himidia Omary wa Kusini Unguja amemalizia nafasi ya tatu na ametumia 59:73.
Aidha mita 100 Winfrida Makenji wa Kaskazini Unguja ameshika nafasi ya kwanza ,huku Siwema Julius wa Pwani ameshika nafasi ya pili 12:68 na Betha Everest wa Kilimanjaro amekimbia 12:94.