MBULU WAFIKA BMT KUJIFUNZA NA KUSHAURIWA
service image
01 Sep, 2023

Wajumbe kutoka Halmashauri ya Mbulu wakiongozwa na Mwenyekiti Mhe. Joseph G. Mandoo wamefika katika Ofisi za Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kujifunza na kupata ushauri kuhusu miundombinu ya Michezo na namna bora ya kuendeleza sekta ya michezo katika eneo lao kulingana na hali ya hewa ya eneo hilo.

Aidha, katika mazungumzo yao na Katibu Mtendaji wa Baraza Bi. Neema Msitha wamefafanua kwa kina hali ya hewa ya Halmashauri hiyo na kuiomba Serikali kupitia BMT kuona fursa ya kupeleka miundombinu ya michezo ili vipaji vingi vya wanariadha na michezo mingine viweze kuibuliwa kwa manufaa ya kulitangaza Taifa Duniani kupitia sekta hiyo.

Mwenyekiti katika ziara hiyo aliambatana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. Abubakar A. Kuuli, Athanas J. Kijuu Afisa Michezo, Damas D. Debwa Afisa Mipango (W) na Nyanda Msirikale Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika Halmashauri hiyo.