MHE. MCHENGERWA AKUTANA NA MAWAZIRI WA AFRIKA MASHARIKI NA UINGEREZA

27 Jul, 2022
Mawaziri wa Michezo wa Tanzania, Kenya na Uganda wakizungumza leo Julai 27, 2022 walipokutana nchini Uingereza katika Mkutano wa Mawaziri wa Michezo wa Nchi za Jumuiya ya Madola.
Mkutano huo, ni moja ya shughuli kabla ya kuanza rasmi kwa michezo ya Jumuiya hiyo, ambapo Tanzania inashiriki katika michezo ya riadha, ngumi za ridhaa, judo, kunyanyua vitu vizito kwa watu wenye ulemavu na kuogelea.