MHE.MCHENGERWA AVITAKA VILABU KUMILIKI VIWANJA.

18 Aug, 2022
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Mohamed Mchengerwa amekutana na Watendaji Wakuu wa Klabu za Ligi Kuu ya NBC Simba SC, Young Africans, Azam FC na Ruvu Shooting kujadili mambo mbalimbali ikiwemo vilabu vya Ligi Kuu kuendelea kuwekeza katika miundombinu hususani umiliki wa viwanja vya kuchezea kwa vilabu hivyo.