MHE. MCHENGERWA AWAPONGEZA WATANZANIA

29 Mar, 2022
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe. Mohamed Mchengerwa leo Machi 29,2022 amewaongoza watanzania kuishangilia timu ya Taifa (Taifa Stars) kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Sudan Kusini.
Mchezo huo umechezwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam kwa timu zote kutoka kwa sare ya goli 1-1.
Mchezo huo ulikuwa ni tukio la kuadhimisha mwaka mmoja wa mafanikio ya Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan katika sekta ya michezo tangu aingie madarakani.
Mhe. Mchengerwa katika tukio hilo aliambatana na Katibu Mkuu. Dkt, Hassan Abbasi na viongozi mbalimbali wa Serikali kushuhudia mpambano huo.