MHE. MCHENGERWA AWATAKA WACHEZAJI KWENDA KULIPAMBANIA TAIFA

20 Jul, 2022
Na. Najaha Bakari -DSM
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa amewataka wachezaji wanaoliwakilisha taifa katika mashindano ya Jumuiya ya Madola nchini Uingereza na michezo ya Afrika nchini Misri kwenda kulipambania taifa kwa kurudi na ushindi katika mashindano hayo.
Hayo ameyasema leo tarehe 20 Julai, 2022 katika hafla ya kuziaga timu hizo zinazoshiriki katika mashindano hayo ya kimataifa.
"Wekeni Uzalendo mbele, nendeni makaliletee taifa heshima,"alisema.
Aidha, amewataka wachezaji hao kuimarisha nidhamu na maadili wawapo katika mashindano hayo
"Twende tukashinde tusiende kutembea," alisisitiza Mhe. Waziri.