MICHEZO YA MAPIGANO YAPAMBA MOTO

16 Jan, 2023
Mashindano ya mchezo ya mapigano (Kickboxing) unatarajiwa kurindima Februari 25, 2023 Jijini Dar es salaam.
Aidha, mashindano hayo yanatarajia kushirikisha michezo tofauti ya mapigano ukiwemo kickboxing yenyewe chini mchezo wa wushu, ngumi, kriketi na michezo mingine ya mapigano.
Akizungumzia mashindano hayo leo Januari 16, 2023 wakati wa mkutano na waandishi wa habari za michezo Sensei Gora amesema, mashindano hayo yanatarajiwa kuwa na wapiganaji zaidi ya mia moja (100) na kuongeza kuwa mwezi machi wanatarajia kuwa na ligi ambayo itahusisha wapiganaji zaidi ya mia tatu (300).
Mkutano huo umefanyika katika klabu ya Fay heroes fitness Mikocheni ambayo ni mmoja wa wadhamini wa mashindano hayo.