MIPANGO KUELEKEA LADIES FIRST 2023

15 Dec, 2022
Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kwa kushirikiana na Shirika la Ushirikiano la Kimataifa la Japani (JICA) wameendelea na mipango mikakati ya mafanikio kuelekea katika mashindano ya mbio za wanawake yajulikanayo kwa jina la (Ladies First) yanayotarajiwa kufanyika mwezi Januari 2023.
Mikakati hiyo ya mafanikio inayotekelezwa na BMT kwa ushirikiano na JICA ni pamoja na kukagua miundombinu mbalimbali itakayotumika wakati wa mashindano hayo.