MLANDEGE YAWATOA KIMASOMASO WAZANZIBAR BAADA YA MIAKA 13
service image
13 Jan, 2023


Timu ya mpira wa miguu ya Mlandege imewatoa kimasomaso Wazanzibar kwa kuibuka kidedea kwa goli (2) na kuchukua ushindi wa kwanza (1) dhidi ya mpinzani wake Timu ya Singida Big Stars walioibuka na ushindi wa pili (2) kwa goli (1).

Ushindi huo umepatikana baada ya miaka (13) ya kombe hilo tangu mwaka 2009 ikiwa ni msimu wa kumi na saba (17) wa kombe la mapinduzi na fainali iliyozikutanisha timu hizo tarehe 13 Januari, 2023 katika Uwanja wa Amani Mjini Zanzibar.

Aidha, mshindi wa kwanza Timu ya Mlandege ameondoka na Kombe, kitita cha Sh. Milioni thelathini (30) na Medali za dhahabu kwa wachezaji wote wakati mshindi wa pili akijinyakulia kitita cha Sh. Milioni ishirini (20) na Medali za fedha kwa wachezaji wake.