MSITHA AITAKA TKSA KUENDELEZA UAMINIFU KWA ST. JOSEPH

Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Neema Msitha ametoa wito kwa Viongozi wa Chama cha mchezo wa Kabaddi Tanzania (TKSA) kuendeleza uaminifu waliojenga kwa Chuo Kikuu St.Joseph ili waendelea kufaidika na udhamini kupitia mchezo wa kabaddi.
Msitha ameitoa kauli hiyo leo tarehe 08 Februari, 2023 wakati akishuhudia utiaji wa saini wa Mkataba wa ushirikiano kati ya TKSA na Chuo Kikuu cha St. Joseph utakaodumu kwa mwaka Mmoja uliofanyika katika ofisi za baraza hilo Jijini Dar es salaam.
Àlisema kuwa Baraza linatamani kuona Chuo wakiona TKSA wanafanya vyema waweze kuongeza vipengele vingine vya ufadhili huo.
"Nitoe wito Chama uaminifu mlioujenga mpaka mkaaminika hadi mmeonekana mkae kuingia makubaliano, tunaamini wenzetu wakiona mnafanya vyema wataimarisha vipengele zaidi, na tumebariki waendelee na mchakato kwani wamefanikiwa kutafsiri sera ya Maendeleo ya michezo,"alisema Neema.
Alitaja vitu ambavyo vipo katika mkataba huo ni pamoja na ofisi ambalo BMT inatikia mkazo kwa vyama viwe na ofisi.
Naye Mwenyekiti wa TKSA Abdallah Nyoni, alitaja makubaliano hayo ni pamoja na kugharamia timu ya Taifa inayojiandaa na mashindano ya Dunia na Afrika Kwa kambi itajayowekwa katika Chuo hicho, gharama za malazi, chakula na usafiri wa ndani watakapokuwa katika majaribio na michuano hiyo.
Àlisema kuwa makubaliano mengine ni kutoa mafunzo kwa makocha na waandishi wa Habari kuhusu Mchezo huo, kuendesha mabonanza mbalimbali ya mchezo huo, kununua mazulia ya kuchezea mashindano ya ndani na nje .
"Hii kwetu ni fursa kubwa sana kwa haya yote, hivyo tunaahidi kuongeza uaminifu Kwa ushirikiano wa uongozi wa Chama ,"alisema Nyoni.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Chuo hicho Profesa Elias Zephania, alisema wanaahidi kutekeleza sehemu ya ushirikiano wa makubaliano hayo.
Alisema kuwa ufadhili wao ni mchango wa ushirikiano katika masuala ya ushirikishwaji kwa jamii.