MSITHA APOKEA UJUMBE KUTOKA JAPANI NA SUDAN KUSHUHUDIA MASHINDANO YA LADIES FIRST
service image
20 Jan, 2023

Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Neema Msitha leo tarehe 20 Januari, 2023 amepokea ugeni kutoka nchini Japan na Sudani Kusini waliofika kwa lengo la kushuhudia mashindano ya riadha ya wanawake yaliyopewa jina la 'Ladies First' yanayofanyika tarehe 21 na 22 Januari, 2023 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es salaam.

Mashindano hayo yanatarajiwa kufunguliwa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dorothy Gwajima ambayo yatahusisha wanariadha kutoka Mikoa 31 ya Tanzania.

Vilevile yatapamba na nyimbo kutoka kwa Msanii Dulla Makabila pamoja na waimbaji wa Roller dance.