MSITHA ATETA NA KAMATI YA MICHEZO YA MAJESHI DUNIANI
service image
30 Jan, 2024

Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bi. Neema Msitha leo tarehe 30 Januari, 2024 amepokea Ujumbe kutoka Baraza la Michezo la Majesho Duniani lililopo Ubeligiji likiambata na wenyeji Baraza la Michezo la Majesho Tanzania ambao wanatarajia kuwa mechi wakati wa mkutano wao muhula wa 79 tarehe 12 hadi 19, Mei, 2024 nchini Tanzania.

Katika kuendelea kudumisha amani duniani kupitia ushiriki kwenye michezo tarehe 16 Mei, wameandaa mechi kati ya Baraza la Michezo Duniani linaloundwa na wajumbe kutoka Bara la Asia, Ulaya, Amerika, na Afrika dhidi ya Kamati ya amani na maridhiano ya Taifa ya Tanzania.

Msitha, kwa niaba ya Serikali amewahakikishia ushirikiano na kuwataka watanzania kuja kwa wingi katika mechi hiyo Mei 16, 2024 Uwanja wa Benjamini Mkapa.

Mgeni rasmi katika mechi hiyo anatarajiwa kuwa Waziri mwenye dhamana ya Michezo Dkt. Damas Ndumbaro, ambapo, mkutano huo unatarajiwa kuwa na wajumbe 300 kutoka nchi 140 wanachama wa Baraza la Michezo ya Majeshi Duniani.