MSITHA - ATOA SIKU 7 KUWASILISHA WAJUMBE WA KAMATI NDOGO CHANETA

Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Neema Msitha ameitaka kamati ya Utendaji ya chama cha netiboli nchini kuwasilisha majina ya wajumbe wa kamati ndogo ndani ya wiki moja.
Amezitaka kila kamati hizo katika vyama vya michezo kutelekeza majukumu yao kwa mujibu wa Katiba ili kuepuka migogoro inayojitokeza mara kwa mara katika vyama hivyo.
Msitha ameyasema hayo leo tarehe 13 Desemba, 2022 wakati wa kikao na Kamati ya Utendaji ya Chama cha mchezo wa Netiboli Tanzania (CHANETA) kusikiliza migogoro inayoendelea katika chama hicho na kukwamisha maendeleo ya mchezo huo nchini.
"Kila kamati ikae na kupanga mipango yake na kuiwasilisha kwa kamati ya utendaji ili kupata baraka kwa ajili ya utekelezaji"
Amewataka kila maamuzi kufanyika ndani ya kikao na kusisitiza ndani ya wiki moja kuwasilisha majina ya wajumbe wa kila kamati hizo.