MSITHA AVITAKA VYAMA VYA MICHEZO KUANDAA MASHINDANO MENGI

Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Neema Msitha amevitaka vyama vya michezo nchini kuandaa mashindano mengi ili kuwajengea uwezo na uzoefu wachezaji, ili waweze kufanya vizuri katika mashindano ya ndani na nje ya nchi.
Msitha ameyasema hayo leo Januari 22, 2022 wakati wa ufungaji wa mashindano ya riadha ya Wanawake "Ladies First 2023" yaliyofanyika kwa siku mbili (2) katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es salaam.
Pia amewaasa wachezaji kuendeleza juhudi katika kufanya mazoezi ili waendelee kujiimarisha zaidi.
"Lengo la mashindano haya ni kuhakikisha tunaongeza na tunahamasisha ushiriki wa wanawake katika michezo, hivyo basi niwaombe wachezaji muongeze juhudi ya kufanya mazoezi, muhakikishe mnatenga muda wa kutosha kwa ajili ya mazoezi,"alisema.