MSITHA AWATAKA VIONGOZI WA SHIMMUTA KUTEKELEZA MAAGIZO YA VIONGOZI

13 Dec, 2022
Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) leo tarehe 13 Disemba, 2022 amekutana na Viongozi wa Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma Tanzania (SHIMMUTA) kujua utekelezaji wa Maagizo ya Viongozi akiwemo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Isidori Mpango aliyotoa wakati wa uzinduzi wa mashindano ya shirikisho hilo tarehe 20 Novemba, 2022 Mkoani Tanga.
Kikao cha Mtendaji wa BMT kimemhusisha Mwenyekiti wa Shimmuta Roselyne Massam na Mjumbe wa Halmashauri Simba Mchunga pamoja na baadhi ya Maafisa wa Baraza.