MSITHA ASISITIZA UWAJIBIKAJI NA UBUNIFU

15 Dec, 2023
Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bi. Neema Msitha amewasisitiza Watumishi kuwajibika na kuwa wabunifu kila mtu katika nafasi yake ili kuongeza ufanisi katika kutekeleza majukumu yao.
Rai hiyo ameitoa leo Disemba 15, 2023 wakati wa kikao na watumishi wa Baraza hilo kilicholenga kupeana taarifa mbalimbali za utekelezaji sambamba na kupanga mikakati ya maendeleo katika taasisi hiyo.
Aidha, kikao hicho pia, kilihudhuriwa na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu kutoka Wizara ya Utamaduni , Sanaa na Michezo Bi. Severa Salvatory ambaye pia amewataka watumishi hao kuzingatia Uaminifu, Uadilifu, Utii na Utendaji kazi katika kutekeleza majikumu yao.