MSITHA: WADHAMINI WEKEZENI KWENYE MICHEZO YA WANAWAKE KUNA NGUVU KUBWA YA KUJITANGAZA.
service image
05 Sep, 2022


        Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Neema Msitha amewashauri wawekezaji kuona fursa kubwa iliyopo ya kuwekeza katika michezo ya wanawake ili kupanua wigo zaidi wa bidhaa zao kutokana na nguvu ya wanawake.

Rai hiyo ameitoa leo Septemba 04, 2022 wakati wa tukio la kufunguliwa na kupandishwa kwa bendera za nchi zaidi ya ishirini (20) zilizowasili Tanzania kushiriki mashindano ya Afrika ya mchezo wa Gofu kwa wanawake unaoanza kesho tarehe 05 hadi 07 na kumaliziwa na mashindano ya ndani hadi Septemba 13 katika viwanja vya Gymkana Jijini Dar Salaam.



"Wadhamini wekezeni kwenye michezo ya wanawake ili itambulike kama ya kiume, lakini pia michezo ya wanawake ina nguvu kubwa,"alisisitiza Msitha.

Naye Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Yusuph Singo aliyefika kifungua mashindano hayo kwa niaba ya Waziri mwenye dhamana ya michezo Mohamed Mchengerwa, amewataka washiriki kuhamasisha jamii nzima katika nchi hizo na kuwaondoa hofu kuwa mchezo huo siyo wa matajiri bali kila mtu anaweza kushiriki.