MWANA FA : TANZANIA ITAKUJA KITOFAUTI
service image
15 Jan, 2025

NAIBU Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo,  Hamisi Mwinjuma ‘Mwana FA’, amesema kusogezwa mbele kwa miezi sita ya maandalizi ya mashindano ya Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) inatoa nafasi kuendelea kuwa bora kwa miundombinu.
Kauli hiyo amesema Jumatano ya Januari 15, kwenye hafla ya Kongamanano la wadau wa Michezo kuelekea CHAN na fainali za AFCON 2027.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) Jumanne , Januari 14, 2025, limetangaza kuahirishwa kwa michuano ya CHAN ambayo ilitakiwa kufanyika Februari 1 hadi 28 lakini sasa kusogezwa mbele hadi Agosti mwaka huu, Tanzania, Kenya na Uganda.
Mwana FA amesema muda wa miezi sita ya maandalizi inatoa fursa ya kujihakikishia mashindano hayo yanakuwa na utofauti mkubwa na kuacha alama nzuri.
“Tanzania tulikuwa tumefika kwa asilimia 90 ya maboresho ya uwanja na kuwa tayari kwa michuano hayo, lakini baada ya kupokea taarifa ya kusogezwa mbele kwa mashindano hayo inatoa muda wa kujipanga vizuri na mashindani hayo kuwa na utofauti na tulivyopanga,” amesema.