KAMATI YA KUCHANGIA TIMU ZA TAIFA YATOA RIPOTI
service image
18 Jan, 2024

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ameipa maagizo matatu Kamati ya Hamasa ya Uchangiaji kwa timu za Taifa juu ya maendelo ya ukusanyaji wa michango iliyohaidiwa na wadau mbalimbali kwa ajili ya timu hizo.

Akizungumza na Waandishi wa habari Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Patrick Kahemele, alitaja maagizo hayo ni kuandaa ripoti ya ahadi na kuwasilisha kwake kila baada ya wiki mbili na kuitaka Kamati hiyo kwenda Dodoma mwisho wa mwezi huu kumpa ripoti namna ya walivyoweza kukusanya ahadi na kupokea ahadi mpya .

Alisema kuwa maagizo mengine kuendelea kufanya promosheni ya kuhamasisha na kuhakikisha wanawafikia wadau wengi zaidi wafanyabiashara wakubwa,wakati kwa kuwafikishia barua ya kuwaunga mkono.

"Tunaomba vyombo vya habari nchini vituunge Mikono katika kwenye jukumu hili la kitaifa ," alisema Kahemele.

Kahemele alisema Kuwa wametuma ombi kwa waziri MKuu waandae hafla ya chakula Kwa wadau waliochangia ambayo itafanyika baada ya mfungo wa Eid wa fitri na Pasaka .

Kahemele alisema katika harambee wamekusanya ahadi za shilingi bilioni 4.27 ambapo tayari milioni 800 zimekusanywa na kuwekwa katika akaunti.

Fedha hizo zitakazopatikana kutoka kwa wadau ni Kwa ajili ya kugharamia timu za Taifa zinazotarajia kushiriki mashindano ya Kimataifa .

Mashindano hayo ya Afrika,.Mpira wa Miguu Kwa watu wenye Ulemavu Afrika , na Olimpiki