TIMU YA MIELEKA YA NAVY WATWAA UBINGWA WA KOMBE LA MKUU WA NAVY

03 Sep, 2023
TIMU ya Mieleka ya Navy imetwaa ubingwa katika mashindano ya Kombe la Mkuu wa Navy yaliyomalizika jana kwenye Ukumbi wa Fukwe ya Navy Dar es Salaam.
Navy imetawazwa bingwa baada ya kujikusanyia pointi 75 akiwa na medali za Dhahabu nne ,fedha tano,huku akifuatiwa na Ngome ambaye alipata pointi 61 akiwa na Dhahabu nne,fedha tatu na Mbagala akimalizia nafasi ya tatu Kwa kujipatia pointi Saba Kwa kupata medali ya fedha moja .