BMT YAMWAGA ZAWADI KWA WASHIRIKI WA SAMIA TANZANITE SUPER CUP
service image
08 Mar, 2025

Yanga Princess imejinyakulia Kombe, fedha taslim shilingi Milioni 3 na medali za dhahabu kwa udhamini wa Baraza la Michezo la Taifa kupitia Tamasha la Tanzanite Women's Festival, huku mshindi wa pili JKT Queens ikijinyakulia shilingi Milioni 2 na medali za shaba.

Mshindi wa tatu Simba Queens ameondoka na Fedha taslim shilingi Milioni Moja na nusu na medali za shaba huku mshindi wa nne Fountain Gate akiondoka na shilingi Milioni Moja.

Amegawa zawadi hizo Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bi. Neema Msitha leo Machi 08, 2025 baada ya sherehe za siku ya wanawake, tukio lililofanyika katika Uwanja wa sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.

Zawadi hizo zimetolewa baada ya kukamilika kwa michuano Samia Women's Super Cup' iliyomalizika tarehe 07 Machi, 2025 katika Uwanja wa Aga Khan Jijini hapo.