MASHINDANO YA KUFUZU OLYMPIC 2024

07 Sep, 2023
Baraza la Michezo laTaifa (BMT) limewaaga na kuwakabidhi bendera mabondia sita wa ngumi za wazi kwenda nchini Senegal kwenye mashindano ya kufuzu kushiriki mashindano ya Olimpiki yanatarajiwa kufanyika nchini Ufaransa 2024.
Akikabidhi bendera hiyo kwa niaba ya Katibu Mtendaji Thadeus Almas Mwanasheria wa BMT amewataka kwenda kuipigania nchi kufuzu kushiriki mashindano hayo na siyo kwenda kutembea.