KUAHIRISHWA KWA KIKAO KAZI"

29 Aug, 2023
Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa Dkt. Emmanuel Ishengoma amefunga Kikao Kazi cha Maafisa Utamaduni na Michezo kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa wa Njombe leo Agosti 29, 2023 mkoani hapo.
Aidha, Dkt. Ishengoma amewasisitiza maafisa hao kwenda kutekeleza maagizo na maazimio ya kikao kazi hicho pamoja na kuongeza tija katika utekekezaji wa majukumu waliyopewa ya kuendeleza Sekta za Utamaduni na Michezo hususani kuibua na kukuza vipaji vya Sekta hizo katika maeneo yao.